Monday , 5th Jul , 2021

Mkurugenzi mpya wa ufundi wa Tottenham Fabio Paratici ameweka wazi kuwa jukumu la kuhakikisha Harry Kane anasalia ndani ya klabu hiyo sio la kwake peke yake bali ni jukumu la klabu kwa ujumla kuhakikisha anasalia klabuni hapo, Kane aliweka wazi kuwa anataka kuondoka klabu hapo.

Harry Kane

Klabu za Chelsea na Manchester City zote za England zimeonyesha nia yakutaka kumsaji Kane, na mwezi uliopita Manchester City ilipeleka ofa ya pauni milioni 100 kama ada ya uhamisho ambayo ni zaidi ya bilioni 321 kwa pesa za kitanzania, lakini ofa hiyo ilikataliwa na Spurs ambao nao hawana nia ya kumuuza.

"Kumbakiza sio lengo langu tu, ni malengo yetu kama klabu, siwezi kusubiri kumtazama akicheza moja kwa moja, nimekuwa na bahati kweli katika miaka iliyopita kwa sababu nimewaona wachezaji wengi wa juu na washambuliaji, kama Cristiano Ronaldo, Carlos Tevez, Alvaro Morata, Gonzalo Higuain, na wengine wengi ambayo sasa nimewasahau. Hivi sasa, yeye ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi ulimwenguni, ni mchezaji kamili.” Amesema Fabio Paratici

Kwa sasa Kane yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya England kwenye michuano ya Euro 2020, na kikosi hicho kimefuzu hatua ya nusu fainali na kitacheza dhidi ya timu ya taifa ya Denmark Julai 7, 2021. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amefunga mabao matatu (3) kwenye michuano hiyo katika michezo mitano (5).

Msimu uliopita Harry Kane alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu England alimaliza msimu akiwa na mabao 23 lakini pia alitwaa tuzo ya mchezeshaji bora baada ya kutoa pasi za usaidizi wa mabao (assist) 14.