Monday , 5th Jul , 2021

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka kiapo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram masaa kadhaa yaliyopita kuwa, endapo Wekundu hao wa msimbazi watafungwa dhidi ya Yanga kwenye fainali ya Shirikisho mkoani Kigoma basi ataacha kazi.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Manara pia ameendelea kwa kuwatupia lawama wachezaji wa Simba kuwa hawajitumi ilhali mashabiki wanatimiza wajibu wao kwa kujaa uwanjani na Uongozi kutimiza wajibu wake. Manara amemuelekeza nahodha John Bocco kuzungumza na wachezaji wenzake na kujitathmini.

Maneno hayo yamekuja siku moja baada ya Simba kufungwa na Yanga bao 1-0 kwenye mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu bara ulichezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 3 Julai 2021.

Manara ameandika;

“Unafika Pemba kutokea Airport hadi kinyasini Wete Pemba kote barabarani watu wametinga jezi za Mnyama. Wapemba hawajali kuhusu matokeo ya juzi,,before sikuwa najua Pemba ina Simba wengi kiasi hiki aiseee."

“Captain @john_22_bocco sema na wenzio bro,,,mtakuja kuua watu Kwa makundi siku moja ,naambiwa Dar kuna Shabiki kajipiga kitanzi huko,,,half ya kwanza mmecheza kama mmelazimishwa au mnadai kitu,,mmezinduka second half na wao wakaweka contena mechi ikaisha,,,,”

“Wallah kigoma tukifungwa naacha hii kazi narudi Shamba kulima,,,,viongozi wanatimiza majukumu yao, Washabiki wanajaa kuliko Washabiki wao kwa mbali mno,,mm natukanwa kutwa Kwa kuwapa nguvu nyie lakini mmeenda kutuangusha,,,,”

“Sioni sababu ya kuendelea na kazi hii kama wachezaji hawajui nn maana ya uzito wa Derby,,,Wachezaji wao wanajitoa asilimia elfu moja toka dakika ya kwanza,,,cc tunazinduka kushakuchwa,,,,kaeni wenyew zungumzeni na thamani ya jezi ya @simbasctanzania ilindwe”.