
Mshindi mara tano wa michuano ya US Open, Rafael Nadal akiwa mchezoni.
Nadal ambaye pia ni bingwa mara tano wa michuano hiyo, amesema uamuzi wa kujitoa kwenye michuano hiyo umekuja baada ya kufuata ushauri kutoka kwa familia yake na jopo la matabibu ambao wamemfanyia vipimo na kugundua nyota huyo anahitiaji muda wa mwaka mzima kujiuguza
Nadal mwenye miaka 35, anaungana na bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Dominic Thiem kutoka Australia ambaye jioni ya jana alithibitisha kuwa hatoshiriki kwenye mashindano hayo baada ya kujitonesha kwenye mkono wake hivyo atakuwa nje pia kwa mwaka mzima.