Wednesday , 25th Aug , 2021

Tume ya Tehama Tanzania, imezindua tuzo za Tehama Nchini, ambapo washiriki wanapendekezwa na Wananchi wanaotumia Teknolojia zinazoendeshwa na wahusika ambao ni makampuni ya simu, Bima, Elimu, Afya, pamoja na mtu mmoja mmoja.

Samson Mwela, Mkurugenzi Tume ya Tehama.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo, Mkurugenzi Tume ya Tehama, Samson Mwela, amesema zoezi hilo linaanza leo Agosti 25, 2021 ambapo wananchi wenyewe watapendekeza.

“ICT Awards itawapa Watanzania wenyewe nafasi ya kupendekeza majina ya Watu au kampuni za watoaji wa huduma bora wa Tehama nchini, ambapo zoezi limezinduliwa leo Agosti 25, 2021 kwenye tovuti ya tume yaani https://www.ictc.go.tz/ hadi Septemba 10” - 

“Baada ya zoezi la kupendeza washiriki kukamilika, Septemba 11-18 waliopendekezwa watajaza fomu Maalum wakieleza nini wamefanya ambacho kilipelekea wakapigiwa kura na Wananchi'' - Samson Mwela, Mkurugenzi Tume ya Tehama.