
Timu ya taifa ya wavu ya Tanzania ilipokuwa inacheza dhidi ya Kenya.
Tanzania inashiriki tena mashindano hayo ya mpira wa wavu mataifa ya Afrika baada ya miaka 44 kwani itakumbukwa kuwa mara ya mwisho walishiriki michuano hiyo mwaka 1977 ilipofanyikia katika mji wa Benghazi nchini Libya.
Mashindano hayo pia yatatumika kwa ajili ya kusaka nafasi ya kushiriki mashindano ya wavu ya Dunia ‘World Championship 2022’ ambapo kila nchi itawakilishwa na timu ya taifa ya wanawake na wanaume. Kwa upande wa wanaume, timu zitakazoshiriki ni wenyeji Rwanda, Burundi, Burkina Faso, Cote D’Ivoire, Cameroon, Congo DR, Misri, Ethiopia, Gambia, Guinea, Kenya, Mali, Morocco, Niger, Nigeria, Sudan Kusini, Zambia, Tunisia, Uganda na Tanzania.
Viongozi wa 'Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania' (TAVA) walichagua kikosi cha wachezaji 15 baada ya kukaa kikao na kulidhiana huku kikosi hicho, kitaongozwa na kocha mkuu, Ally Mohamed kutoka Police Zanzibar akisaidiwa na Nasoro Sharifu wa Jeshi Stars.
Wachezaji waliotwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na (Setters) Ezekiel Rabson, Nassoro Mohamed (Jkt), Dismas Dick (Magereza). I Middle Blockers) Ramadhan Mase (Chuff), Abdulhaman Yusuf (Jeshi). Deodatus Baitubaki (Jkt), Michael N’gonge (Jeshi). (Receiver Attackers) David Evarist (Equity Bank, Kenya), Joseph Mafuru (Jeshi), Khantis Sadala (Mafunzo Zanzibar), Ford Edward (Tanesco), (Opposite) Shabani Julius (Chul), Jackson Mmari (Rukinzo Police, Burundi) pamoja na (Liberos) Rashid Mustapha (Jkt) na Said Ali (Mafunzo Zanzibar).