Friday , 3rd Sep , 2021

Toto Badi Marioo anasema kwa wasanii wa kizazi chake hakuna wa kushindanishwa naye kwa kuangalia vigezo vya ngoma kali za back to back na uandishi kwa ujumla.

Picha ya msanii Marioo

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Marioo anasema hataki kuwaweka wasanii waliomtangulia kwa sababu atakuwa anajilinganisha nao ila kwa kizazi chake haoni wa kumfikia.

"Nikiangalia kwenye 'generation' yangu sioni wa kumuweka kwa kuangalia hits zake na zangu toka nianze mimi nafumua tu, japokuwa nao wanafanya vizuri, wanasizi na wanaibuka tena"

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.