Monday , 6th Sep , 2021

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 33 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Fikosh kuacha njia na kupinduka jana jioni Septemba 5, 2021, katika mteremko wa Nyangoye ulioko katika Manispaa ya Bukoba mkoani wa Kagera.

Basi la Kampuni ya Fikosh lililopata ajali mkoani Kagera

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Machali, amesema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T710 BXB, linafanya safari zake kati ya mkoa wa Kagera na Mwanza na kwamba wakati linapata ajali lilikuwa likitokea mkoa wa Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea vifo hivyo na kwamba miongoni wa waliopoteza maisha watatu ni watu wazima na mmoja ni mtoto mdogo.