Wednesday , 8th Sep , 2021

Mchezaji chipukizi wa tenisi Leylah Fernandez amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya US Open baada ya kumshinda Elika Svitolina, kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Arthur Ashes, New York.

Leylah Fernandez, akishangilia ushindi wake kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano ya US Open baada ya kumshinda Elina Svitolina

Fernandez ambaye alitimiza umri wa miaka 19 siku ya Jumatatu, alionesha jitihada zote kushinda mchezo huo kwa seti ya 6-3, 3-6, 7-6, (7-5) ambapo atacheza dhidi ya Aryan Sabalenka kwenye hatua ya nusu fainali.

Mchezaji huyo chipukizi kutoka Canada amemshinda bingwa mtetezi Naomi Osaka, mshindi wa 2016 Angelique Kerber na sasa mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki Svitolina katika mbio yake ya nusu fainali ya kwanza. Nyota huyo ndiye mwanamke chipukizi zaidi kufikia nusu fainali ya wazi ya Amerika tangu Maria Sharapova mnamo 2005, akifika hutua hiyo siku moja baada ya siku yake ya kuzaliwa.

Nyota huyo ndiye mwanamke chipukizi zaidi kufikia nusu fainali ya wazi ya Amerika tangu Maria Sharapova mnamo 2005, akifika hutua hiyo siku moja baada ya siku yake ya kuzaliwa.