Wednesday , 15th Sep , 2021

Wananchi wa Vijiji vya Halawa na Ihusi Bariadi mkoani Simiyu, wamelalamikia kitendo cha wanafunzi wanaosoma shule za msingi katika vijiji hivyo vilivyopo pembezoni, kutumikishwa kazi za ndani na baadhi ya walimu ikiwamo kufua nguo na kuwapikia chakula, jambo linalotakiwa kudhibitiwa haraka

Baadhi ya wananchi Vijiji vya Halawa na Ihusi Bariadi mkoani Simiyu

Malalamiko hayo yametolewa kwenye mikutano ya hadhara katika vijiji hivyo, ambapo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 pamoja na itifaki za kikanda, zinazuia utumikishwaji wa watoto na kutoa kipaumbele cha elimu.

Kulingana na malalamiko ya wananchi, Diwani wa Kata ya Nkindwabiye, Safari Ng'habi, ametangaza uchunguzi juu ya suala hilo, huku Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Lupakisyo Andrea Kapange, naye akatoa onyo kwa walimu wanaowageuza wanafunzi kuwa vijakazi wao.