Wednesday , 15th Sep , 2021

Muonekano mpya wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un umewa-surprise watu wengi baada ya kuonekana amepungua sana tofauti na alivyokuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Picha ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un

Akiwa amevalia suti ya rangi ya kahawia wakati akikagua gwaride katika kusheherekea miaka 73 ya kuanzishwa Korea Kaskazini, Kim alionekana akiwa na mwili tofauti na uliokuwa umezoeleka.

Kim amekata kilo 20 kama sehemu ya kuboresha afya yake na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uzito kupitiliza.