Thursday , 16th Sep , 2021

Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu (Mahakama ya Mafisadi) inatarajia kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe,

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mahakamani

kesho Septemba 17,2021 baada ya shahidi Kamanda wa Polisi Kinondoni, Ramadhan Kingai kumaliza kutoa ushahidi huo.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Jaji Mustafa Siyani baada ya Upande wa Mashitaka ukiwakilishwa na Wakili, Robert Kidando kumuhoji baadhi ya maswali Kingai ikiwemo kwanini mshtakiwa wa Pili (Adam Kasekwa) hakuhojiwa Arusha alipokamatiwa badala yake wakaja kumuhoji Dar es Salaam.

Katika majibu yake Kingai amesema kulikuwa na upelelezi mwingine uliokuwa ukiendelea Moshi kumuhusu mshitakiwa Mohammed Lingwenya, hivyo wakashindwa kumuhoji mtuhumiwa akiwa Moshi Central Police.

Baada ya kumaliza kumuhoji Upande wa Mashitaka umeomba kesi hiyo iaharishwe hadi Septemba 17 kwa ajili ya kuendelea na shahidi mwingine ndani shauri dogo lenye mashahidi 7.