Thursday , 16th Sep , 2021

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimemsimamisha kazi Rais wa chama hicho Leah Ulaya, baada ya kushindwa kusimamia katiba na kanuni za chama hicho.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya, aliyesimamishwa

Akizungumza na wanahabari Kaimu Rais wa chama hicho Dinah Mathaman, amesema Leah Ulaya, atajadiliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika Desemba 2022.