Thursday , 23rd Sep , 2021

Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amesema kikosi cha wekundu hao kwasasa kinauwezo wa kufanya vyema zaidi licha ya kuwa kuna kazi inahitajika kufanywa ili kuendeleza ubora ulio

Emmanuel Okwi akiwa katika majukumu ya timu yake ya Taifa

Okwi ambaye hivi karibuni alihudhuria kwenye Tamasha la Simba Day akiwa kama mgeni mualikwa, amesema licha ya kuwa na wachezaji wapya, lakini kazi inapaswa kufanyika ili kuendeleza mazuri yaliyofanywa na wachezaji waliopita.

Nahodha huyo wa Uganda The Cranes aliyecheza kwa mafanikio makubwa kwa wekundu hao kuanzia mwaka 2010-2013 kabla ya kuondoka na kurejea tena  2014-2015 kisha 2017-2019, amesema hana cha kuwaambia wachezaji cha kufanya kwakuwa wao wanajua majukumu yao hivyo anaamini wataisaidia Simba kuendelezea ushindani waliouonyesha enzi alizokuwepo klabuni hapo.

''Simba ni timu ya ushindani, ni kweli inawachezaji kadhaa wageni na inahitajika kazi ifanyike kuijenga timu nzuri na ninaamini watafanya vizuri sana ''Alisema Emmanuel Okwi.

Kuhusu Jonas Mkude,Ibrahim Ajibu ambao ni miongoni mwa wachezaji aliocheza nao kabla hajaondoka, Okwi amesema hana cha kuwashauri kwakuwa ni wachezaji wazoefu na wanajua nini Simba inahitaji hivyo watafanya jitihada katika kuhakikisha wanaipa mafanikio klabu hiyo.

Nyota huyo amekuwa akihihusishwa kurejea Msimbazi ingawa hadi sasa bado anamkataba na Klabu ya Al Ittihad ya Misri.