
(Anthony Davis akiugulia baada ya kupata maumivu ya kidole gumba).
Davis aliambulia kucheza dakika 7 pekee na kukusanya alama 2, rebound 3 bila kutoa assist baada ya kupata majanga hayo yaliyompelekea atolewe uwanjani na kushindwa kurejea na timu yake ya Lakers kufungwa kwa alama 105-90 dhidi ya Portland Trail Blazers.
Kipigo hicho kwa Lakers ni majnaga mengine, kwani wamerekodi kipigo chao cha tano kwenye michezo yao kumi ya mwanzo kwenye msimu huu mpya wa NBA wa mwaka 2021-2022 ilhali kikiwa ni kipigo cha 11 katika michezo yake 16 kwa kujumuisha na vipigo 6 mfululizo vya NBA Pre-Season.