
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abas amesema, Serikali itatoa ndege kwa ajili ya mchezo huo ikiwa ni kuhakikisha timu inafanya vizuri nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
“Labda tu niwaambie Serikali katika kuhakikisha tunasapoti michezo tutatoa ndege ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mchezo huo, ndege hiyo itabeba wachezaji na benchi lote la ufundi, viongozi, wadau wa soka na waandishi wa habari kwa lengo la kwenda kuhabarisha watanzania,'' amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Madagascar.
“Tayari tumeshaanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Madagascar, lengo ni kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Kidao huku Taifa Stars inaongoza Kundi J ikiwa na alama 7 sawa na Benin huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na DR Congo wenye alama tano.