
Wanandoa waliohukumiwa miezi 30n jela
Video ya wapenzi hao wawili ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadaye walikamatwa na jeshi la polisi nchini humo na kufikishwa mahakamani.
Wanandoa hao Paskari Hafashimana (29), na mpenzi wake Colodine Mukamulenzi Muhawenimana (24), walionekana kwenye video hiyo wakifanya tendo hilo kwenye barabara ya Kisoro-Bunagana.
Wakisomewa mashtaka yao wanandoa hao walikubali kutenda kosa hilo na waliomba wapunguziwe adhabu, lakini Hakimu aliamuru wafungwe jela kwa muda wa miezi 30.
Chanzo: Tuko swahili