Thursday , 18th Nov , 2021

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amewasisitiza watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kufanya kazi usiku na mchana na wahakikishe kwamba mgao wa maji unatolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

Maelekezo hayo amewapa usiku wa kuamkia leo Novemba 18, baada ya kutinga kwenye ofisi za DAWASA kwa lengo la kutoa maelekezo kufuatia tatizo la upatikanaji wa maji na kuitaka mamlaka hiyo kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari (bowsers).