Sunday , 21st Nov , 2021

Baada ya kushinda mechi 1 kati ya 7 za mwisho kwenye Premier League Manchester United imemfukuza Ole Gunnar Solskjaer.

Ole Gunnar Solskjaer

Baada ya kumfukuza Ole Gunnar Solskjaer, Manchester United imesema timu itakuwa chini ya Michael Carrick kwa muda mfupi wakati wanatafuta kocha wa muda kwaajili ya kumalizia msimu 2021-22.

Solskjaer alichukua mikoba ya Mourinho Disemba 2018, kama kocha wa muda kabla ya kuwa kocha mkuu Machi 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu ambao pia Julai mwaka huu aliongeza mwaka mwingine hadi 2024.