
(Kikosi cha SImba SC cha msimu huu wa mwaka 2021-2022)
Hitimana amesema: "Katika mchezo waliocheza ugenini dakika nyingi wanaonekana ni watu wa kuzuia wanapokuwa ugenini jambo ambalo tunatakiwa kuwaandaa wachezaji watakaocheza mchezo wa aina hiyo hali ambayo tulikutana nayo katika mchezo wa ligi dhidi ya Namungo"
"Hata katika maisha umheshimu mpinzani wako na uende naye sawa, sisi tunatakiwa kufanya hivyo ili tufanye vizuri nyumbani sana na wachezaji wangu. Red Arrows tumewaanggalia na bado tunaendelea kuwaangalia, sio wabaya, ni timu nzuri sana, tunatakiwa kuoambana na kutumia vema dakika 90 nyumbani" Amesema Hitimana.
Baada ya kusema hayo, Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa upande wa Wanachama, Muhtaza Mangungu amesema wamejiandaa vizuri kuelekea kwenye mchezo huo huku wakiwa na tahadhaari kubwa ili wasirudie makosa.
Muhtaza amesema: "Tumejiandaa vizuri na mechi hii tunajua michuano hii ni migumu, kwa sababu timu nyingi zinazotolewa kwenye ligi ya mabingwa zinapokuja huku. Mara nyingi zinazokwenda hadi nusu fainali, fainali na kuchukua ubingwa. Kwahiyo tumejiandaa kukubaliana na ugumu huo. Tunawaomba wanachama na mashabiki wetu wajitokeze waipe nguvu timu yao"
Simba inataraji kushuka dimbani saa 10:00 jioni Jumapili Novemba 28, 2021 kukipiga na Red Arrows ya Zambia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Simba na Red Arrows watarudiana Disemba 5, 2021 nchini Zambia kumsaka mshindi wa jumla atakayetinga hatua ya Makundi.