
(Mshambuliaji wa Royal Antwerp, Mbwana Samatta)
Sare hiyo imeifanya Royal Antwerp iwe na alama 2 tu kwenye michezo yake 5 na kushika mkia wa kundi D nyuma ya Fenerbahce yenye alama 5, ya pili Olympiacos yenye alama 9 na Frankfurt akiwa kinara na alama 11.
Bao hilo la Samatta kufunga mabao 3 kwenye michezo 5 aliyoicheza kwenye michuano hiyo na kuanza kurejesha kiwango chake cha ufungaji lakini timu yake haijafanikiwa kusonga mbele hatua ya mtoano inayofuata ya 32 bora ya Europa.
Kinara wa kundi hilo, Frankfurt amefuzu hatua inayofuata ya mtoano ya 32 bora wakati Royal Antwerp na Fenerbahce zikiwania kumaliza kwenye nafasi ya tatu ili zicheze Uefa Europa Conference Ligi ili zisiambulie patupu.