
(Kocha wa Spurs, Antonio Conte akiwa mazoezini na wachezaji wake)
Spurs wanakabiliwa na michezo miwili ndani ya wiki hii, Alhamisi dhidi ya Rennes ya Ufaransa kwenye mchezo wa kombe la Ligi ya Europa na siku ya Jumapili Disemba 12, 2021 kucheza dhidi ya Brighton kwenye uwanja wa Amex kwenye mchezo wa EPL.
Kwa mujibu wa sheria za UEFA, kama kuna wachezaji 13 hawana maambukizi akiwemo golikipa katika majina 25 yaliyosajiliwa na klabu kwenye michuano hiyo watalazimika kucheza mchezo huo dhidi ya Rennes, ambao ni muhimu kwa Spurs kushinda ili kufuzu hatua ya 32 bora ya michuano hiyo.
Tayari UEFA ilishatoa maelekezo ya michezo yote ya hatua ya makundi kumalizika kabla ya December 31 huku taarifa za ndani kutoka klabu ya Tottenham Hotspurs wakisubiri vipimo vya PCR vinavyotoka baada ya masaa 24