
(Serena Williams (kushoto), Rafael Nadal (katikati) na Novak Djokovic (kulia).
Jina la nyota huyo anayeshikilia nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora duniani kwasasa, limezua taharuki kwani inaaminika hajapata chanjo ya Covid-19 ilhali utaratibu wa michuano hiyo iko wazi kuwa asiyechanja haruhusiwi.
Taarifa kamili kama nyota huyo aliyeamua kushikilia msimamo wake wa kutochanja, kama atashiriki au kutoshiriki kwenye michuano hiyo linasubiriwa kushuhudiwa na wanamichezo Ulimwenguni.
Djokovic anashikilia rekodi sawa na Roger Federer pamoja na Rafael Nadal kwa kuwa wachezaji pekee wenye Grand Slams nyingi, mara 20 hivyo yeyote kati yao ataweka rekodi ya kipekee na kuwapiku wenzake akipata ubingwa mwingine.
Mbali na jina hilo maarufu ambalo halina uhakika wakuwepo, lakini tayari Roger Federer (Grand Slams 20), bingwa wa mwaka 2014 wa Australian Open, Stanislas Wawrinka na Serena Williams (Bingwa mara 7 Australian Open) hawatokuwepo kutokana na kuuguza majeraha yao.
Lakini, Bingwa wa US Open, Emma Raducau (Miaka 18), Cameron Norrie, Dan Evans na Heather Watson ni majina na wacheza tennis wa England maarufu waliothibitisha ushiriki wao kwenye michuano hiyo Januari 17, 2022 Australia.
Licha ya vuta nikuvute ya Djokovic kushiriki au kutoshiriki, lakini James Merlino Kiongozi wa jimbo la Victoria nchini Australia ameendelea kushikilia msimamo wa serikali kwa kusema mchezaji asiye chanja hatoruhusiwa kushiriki.