
(Nyota wa LA Lakers, Lebron James)
Lebron ambaye mwezi ujao atatimiza miaka 37, yupo nyuma ya wakali wafuatao wenye ‘Tripple-double’ nyingi zaidi, Jason Kidd (107), Magic Johnson (138), Oscar Robertson (181) huku kinara akiwa RussellW Westbrook (189).
Kwa upande mwingine, timu yake ya Lakers inaendelea kuwa na mwanzo usioridhisha kwa upande wao, kwani kwenye michezo 26 ya msimu huu wa NBA wamepata ushindi michezo 13 na kufungwa 13.