
(Joash Onyango wa Simba akiwania mpira na Fiston Mayele wa Yanga)
Tokea msimu wa mwaka 2017-2018 hadi msimu wa mwaka huu wa 2021-2022 tayari wameshacheza michezo 9 pamoja na sare ya leo huku Simba ikishinda michezo miwili, Yanga ikishinda miwili na kutoka sare michezo mitano.
Yanga imesalia kuwa kinara wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania kwa kufikisha alama 20 utofauti wa alama 2 na watani wao Simba wenye alama 18 wakiwa na rekodi nzuri ya kutopoteza hata mchezo mmoja kwenye michezo 8 waliyocheza.