
(Kevin Durrant akiwa na mpira na kujaribu kumpita mlinzi wa Detroit Piston)
Kwenye ushindi huo, Durrant amefunga alama 51, rebound 7 na assist 9 na kumfanya Durrant kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu wa NBA kufunga alama nyingi zaidi 51 na kumpiku Stephen Curry wa Warriors aliyefunga 50.
Ushindi huo pia umewafanya Nets wazidi kuwa kileleni mwa Eastern Conference wakifuatiwa na mabingwa watetezi Milawaukee Bucks. kwa upande mwengine, LA Lakers wamepata ushindi wa alama 106-94 dhidi ya Orlando Magic.
NBA itaendelea tena Usiku wa kuamkia kesho huku macho yote yakielekezwa kwa Stephen Curry ambaye amebakisha kufunga 3-pointers 7 ili aifikie rekodi ya gwiji Rey Allen ambaye anaongoza kwenye hostoria ya NBA akiwa na 2,973.
Golden State Warriors ya Stephen Curry itacheza na Indiana Pacers saa 9:00 usiku wa kuamkia kesho Disemba 14, 2021.