Tuesday , 21st Dec , 2021

Nyota wa Brooklyn Nets, Kyrie Irving yu mbioni kurejea kwenye Ligi ya kikapu nchini Marekani NBA baada ya kuwa nje ya ligi hiyo tokea Oktoba mwaka huu kufuatia kugoma kupata chanjo ya Covid-19.

(Nyota wa Brooklyn Nets, Kyrie Irving)

Akielezea uamuzi wa kumrejesha Irving kikosini, Meneja wa Brooklyn, Sean Marks amesema hivi sasa wana wachezaji nane waliopo karantini akiwemo James Harden hivyo hawana wachezaji wakutosha kusaidiana na Kevin Durant ili kulinda usukani walioushika ukanda wa Mashariki.

Licha ya Brooklyn kumrejesha nyota huyo, lakini imeeleza kuwa Kyrie atacheza michezo ya ugenini kwa kuwa bado hajakubali kupata chanjo ya Covid-19 jambo ambalo ni kinyume na taratibu za jiji la New York City iliyopo timu hiyo.