Wednesday , 22nd Dec , 2021

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kufuatia kifo cha mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Magreth Mashue, na kusema kwamba uchunguzi wa awali wa daktari umebaini kwamba shingo ya marehemu ilivutwa.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro Ralph Meela

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro Ralph Meela, na kusema kwamba waliyemkamata ni mwanachuo mwenzake aliyekuwa akiishi naye.

Imeelezwa kwamba Magreth alipotea Desemba 14 hadi Desemba 18 mwili wake ulipopatikana katika mashamba ya chuo hicho.