Saturday , 22nd Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wana Kilimanjaro kwa mapokezi yao kwake na kusema mwanzo walimwimbia kama Simba jike lakini mara baada ya kuvikwa vazi rasmi la mkoa huo akawa Chui jike.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 22, 2022, mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni lililofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi mkoani humo.

"Nashukuru sana nimepata mapokezi mazuri nimetunukiwa vazi hili, waimbaji walisema mimi ni Simba jike, lakini kwa vazi hili kumbe ni Chui jike, lakini inanipa faraja kwamba kuna Chui dume, Chifu Marealle naye amevaa vazi hilo hilo," amesema Rais Samia