Wednesday , 23rd Feb , 2022

Ligi kuu soka Tanzania bara NBC Premier League raundi ya 15 inahitimishwa leo kwa mchezo mmoja, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Yanga SC katika uwanja wa Manungu Complex Turiani mkoani Morogoro. Mchezo huu unachezwa Saa 10:00 Jioni.

Yanga ilishinda michezo yote miwili ya msimu uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar

Vinara wa Ligi Yanga wanaingia kwenye mchezo huu rekodi zikiwa zinawabebe mbele ya Mtibwa saugar, katika michezo 5 ya mwisho Yanga kashinda mara 3 ikiwemo michezo yote miwili ya msimu uliopita ambayo walishinda kwa bao 1-0, wametoka sare mchezo 1 na Mtibwa wameshinda mara 1.

Kwenye msimamo wa Ligi Mtibwa wapo nafasi ya 15 wakiwa na alama 12 katika michezo 14, na wameshinda mchezo 1 tu kwenye michezo yao 5 ya mwisho, wakati Yanga wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 5 wakiwa na alama 36 na kwenye michezo 5 ya mwisho wameshinda 4 na sare 1.

Lakini pia kuelekea mchezo huu Yanga itawakosa Abdallah Shaibu Ninja, Dickson Job na Jesus Moloko wakati wachezaji Djuma Shaaban, Mustapha Yassini na Denis Nkane wato wemerejea kwenye kikosi baada ya kumaliza adhabu na kupona majeruhi.