Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Kibaha mkoani Pwani na kusema kwamba lengo la ujenzi wa chuo hicho ni kutaka chama cha CCM kiwe na viongozi walioandaliwa vizuri na kuishi katika ulimwengu unaobadilika na kwenda na dunia inakoelekea.
Aidha Rais Samia akazungumzia uwepo wa vyama vilivyoanzishwa bila ya uwepo wa itikadi za kueleweka, na hata CCM kuajiri watu bila kuangalia wala kupimana nani anastahili kukaa wapi na nani hastahili katika eneo lipi.


