Friday , 4th Mar , 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema kwamba wao hawana nia na wala hawajapanga kuishambulia nchi ya Urusi na kuyataka majeshi ya Urusi kuondoka nchini kwake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

Rais Zelensky  ameongeza kwamba njia pekee ya kumaliza vita nchini Ukraine ni kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Vladimir Putin wa Urusi.

"Hatutaki kuishambulia Urusi na hatupangi kushambulia, mnataka nini kutoka kwetu?, tokeni kwenye ardhi yetu, njooni tuketi pamoja, msikae umbali wa mita 30, kama alivyofanya wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipokutana na Putin," amesema Rais Zelensky