
(Mshambuliaji wa timu ya Wanawake ya Simba Princess, Opah Clement )
Mshambuliaji hatari wa timu ya Wanawake ya Simba Princess, Opah Clement anataraji kuanza majaribio ya mwezi mmoja kuanzia mwezi huu Machi 2022 kwenye klabu ya Kayserispor Girl ya nchini Uturuki na kama akifanikiwa basi atajiunga na wakali hao wa Uturuki.
Baada ya kupata ruhusa ya kwenda nchini Uturuki kufanya majaribio hayo, Opah ameushukuru Uongozi wa Simba SC kwa kumpa ruhusa hiyo ili kumsaidia kutimiza maono yake.
"Naushukuru Uongozi wa klabu ya Simba Kwa kuniruhusu kwenda kufanya majaribio. Ndoto yangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi" amesema Opah.
Opah Clement ni mshambuliaji tishio na tegemezi kwenye kikosi cha Simba SC hivi sasa, kwani amefunga mabao 19 kwenye michezo 11 aliyocheza kwenye Ligi kuu ya Wanawake nchini Tanzania ‘Serengeti Premier League’.