Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo hii leo Machi 8, 2022, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Maisara visiwani Zanzibar.
"Tumeanza kusikia minong'ono, maisha yamekuwa magumu, kila kitu kinapanda bei ni hao viongozi wetu tulionao hawana baraka, si baraka ya kiongozi ni hali ya ulimwengu inavyokwenda, mafuta yanapanda bei duniani na bidhaa zote zitapanda bei," amesema Rais Samia.






