Thursday , 28th Apr , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya Royal Tour utakaofanyika leo April 28/2022.

Rais Samia ameeleza baadhi ya mambo aliyoyafanya nchini Marekani wakati akizindua filamu hiyo nchini humo.

Hizi ni baadhi ya nukuu za Rais Samia akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kumpokea
"Uhusiano wetu na Marekani mpaka mwaka jana umetimiza miaka 60, lakini tukaona haja sasa ya kubadilisha muelekeo wa uhusiano, huko zamani ilikuwa ni kunyoosha mikono ytunaomba kile na hiki lakini sasa pamoja na kwamba hayo yatakuwepo lakini uhusiano mkubwa sasa ni uwekezaji na biashara" 

"Uhusiano wetu sisi na serikali ya Marekani umekwenda vizuri, tumenyoosha palipokuwa na changamoto kidogo na sasa tupo vizuri tunakwenda nao vizuri sana" 

"Kwa wale wote walio kwenye sekta ya utalii wajipange vyema kupokea wageni, na kuwahudumia ili wapende kuja na kuja zaidi lakini sio kuja tu waongeze na siku za kukaa ndani ya nchi" 

"Sasa watanzania kazi ni kwetu kuwapokea wawekezaji hao bila kuwapa usumbufu, na kufanya uwekezaji wao uwepo Tanzania, ili tutengeneze kazi na tumekisia kama wawekezaji wote tuliosaini nao watakuja tutakuwa tumetengeneza kazi laki tatu na elfu moja na nyingine za juu kidogo"

Unaweza kutazama video hii --