
Bastola
Imeelezwa kwamba tukio hilo limetokea jana Mei 2, 2022, majira ya mchana, baada ya mtoto huyo kuchukua bastola hiyo iliyokuwa imefichwa kwenye sanduku salama mara tu baba yake alipoondoka nyumbani baada ya kumhoji kwanini hakwenda shule licha ya kupewa pesa.
Memusi alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne, katika Shule ya Upili ya Kericho, na polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu iliyopelekea mtoto huyo kujitoa uhai.