Sunday , 8th May , 2022

Mnadhimu Mkuu Wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania-JWTZ,Luteni Jenerali Mathew Mkingule ameipongeza Klabu ya Gofu Ya Lugalo pamoja na familia kwa kuandaa shindano la "Galinoma Memorial Tournament" lililofanyika Kwenye Klabu hiyo Jijini Dar es salaam.

Mnadhimu Mkuu Wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ,Luteni Jenerali Mathew Mkingule (Upande wa kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa jumla Nsajingwa Mwansasu (Upande wa kulia) Kwenye Hafla ya kufunga Shindano la kumuenzi aliyekuwa Mwenyekiti Wa klabu ya Lugalo Gofu Marehemu Brig.Jenerali Mstaafu Ernest John Galinoma "Galinoma Memorial Tournament" Lililofanyika Kwenye Klabu hiyo Dar es salaam.

Shindano hilo lilikuwa na lengo la kumuenzi na kutambua juhudi za kukuza mchezo wa Gofu Tanzania,aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo marehemu Brig.Jenerali Mstaafu Ernest John Galinoma.

Akizungumza kwenye hafla ya kufunga Shindano hilo Mnadhimu Mkuu Wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania-JWTZ, Mathew Mkingule Wakati akimwakilisha mlezi wa klabu hiyo, mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Salvatory Mabeyo, Amesema kumbukizi hiyo inatija kwa familia pamoja na wanagofu wote nchini katika Kuendeleza mchezo huo.

Naye kwa Upande wake Mwenyekiti wa sasa wa klabu ya Lugalo Gofu Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo amesema kwa kutambua mchango mkubwa uliowekwa na muhasisi wa mashindano hayo Jenerali Ernest Galinoma watendelea kushirikiana na familia katika mambo mbalimbali katika kuuendeleza mchezo huo Gofu.

Akizungumza mara baada ya kuibuka Kinara Wa Shindano hilo la "Galinoma Memorial Tournament" Nsajingwa Mwansasu kwa kupiga mikwaju 69,ameshukuru wachezaji wenzie kwa kumpa changamoto ya kiuchezaji iliyopelekea kuwa Mshindi wa jumla wa shindano hilo.

Wachezaji wengine walioibuka na ushindi Divisheni A ni Peter Fiwa aliyepata pointi 73 na Steven Chuwalo pointi 73, divisheni B ni Maliceri Lubuva pointi 71 na Winston Kaunga pointi 73, Divisheni C Sigfrid Urasa pointi 77 na V.Magare Pointi 79, kwa Upande wa senia Said Nkya pointi 75 na Joseph Mbilinyi 80,Huku Upande wa wanawake Habiba Juma pointi 67 na Vick Elias Pointi 80,Mikwaju ya mbali kwa kwa wanaume Likuli Juma na na Upande wa wanawake Ayne Magombe.