Thursday , 19th May , 2022

Dallas Mavericks watakuwa na kibarua kizito kwenye mchezi wa marejeano dhidi ya Golden State Warriors katika dimba la Chase Center siku ya Jumamosi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kati ya  saba inayotarajiwa kuchezwa kwenye fainali ya Kanda Magharibi.

Mchezaji wa Golden State Warriors, Wardell Curry akimzua nyota wa Dallas Mavericks, Luka Doncic.

Wardell Curry maarufu kama Steph Curry alikuwa mwiba mchungu kwa vijana wa Jason Kidd akifunga vikapu 21 ribaundi 12 na pasi za mwisho 4 kwenye ushindi wa 112-87 katika mchezo ambao ulitawaliwa na mbinu za ulinzi kwa pande zote mbili huku Warriors wakifaidika zaidi.

Wachezaji saba wa Warriors walifunga alama 10 hadi 21 na kuwapa wakati mgumu Mavericks chini ya nyota wake Luka Doncic aliyeandika alama 20 pekee huku wachezaji wengine watatu wa dallas wakifunga walau vikapu 10 ambavyo vilikuwa havitoshi kuwapa ushindi .

Kabla ya mchezo wa leo, Dallas walikuwa na rekodi wastani wa kufunga vikapu 105.8 kwa kila mchezo huku wakiwa na tofauti ya wastani wa alama 9.6 kwenye kila ushindi wa michezo hiyo kabla ya kukutana na kipigo kutoka kwa Warriors.