Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, George Kyando
Ambapo kufuatia kifo hicho, wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kwenda kuvunja ofisi ya kitongoji, nyumba ya Mwenyekiti na kuchoma moto pikipiki ya Kamanda wa sungusungu kwa madai ya kuchoshwa na manyanyaso ya viongozi wao.
Kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Namba 2 Shaban Zoro, akakanusha madai yaliyotolewa na wananchi, huku Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi, akauvunja uongozi wa Kitongoji cha Namba 2 na Jeshi la jadi sungusungu.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga George Kyando,amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuharibu mali za umma.