Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TARURA yaagiza kujengwa daraja la dharura Katavi

Thursday , 19th May , 2022

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff ametembelea daraja la Kaseke lililoharibiwa na maji ya mvua na kumuagiza meneja wa TARURA Mkoa wa Katavi Mhandisi Innocent Mlay, kujenga daraja la muda kwa haraka ili wananchi wasipate usumbufu kupita.

Mhandisi Seff ametembelea daraja hilo linalounganisha Vijiji vya Kaseke , Mbugani na Itenka Kata ya Kaseke, Mpanda  katika ziara yake Mkoani Katavi na kukuta wananchi wakilipishwa kiasi cha kati ya shilingi 100 - 500 kwa siku kuvuka katika kivuko kilichojengwa na baadhi ya wanakijiji.

Aliwataka kusitisha maramoja tozo wanayowalipisha wananchi na kumuagiza Mhandisi Mlay  kurudisha gharama ya shilingi 1,500,000 waliyodai ni pesa iliyotumika  kujenga kivuko hicho ili wananchi wavuke bila kulipa.

“Nimesikitishwa kuona wananchi hasa wakinamama wanalipishwa kuvuka hapa,  sasa msitishe maramoja kuwalipisha na meneja atarudisha hizo gharama mlizosema,”alisema Mhandisi Seff.

Aidha alimuagiza meneja Mkoa kujenga daraja la muda kwa haraka wakati ufumbuzi wa kujenga daraja la kudumu unafanyiwa kazi.

“Kama mnavyoona uharibufu uliotokea hapa ni mkubwa hivyo daraja lakudumu litachukua muda kidogo, tutajenga daraja la muda ili muweze kuvuka kwa usalama zaidi, “ alisema Mhandisi Seff.

Kwa upande wao wananchi wa Kaseke wa waliushukuru uongozi wa TARURA kwa kutembelea eneo hilo, na kuleta suluhisho la adha kubwa walizokuwa wanazipata.
 
“Tunakushukuru sana kiongozi ulivyofika hapa, kwa kweli adha tunazopata ni kubwa sana, wakinamama hapa tunapata shida ya kwenda zahanati na watoto na tukivuka hapa tunalipishwa, sasa tunafurahi umesema tusilipe na pia mnatujengea daraja hilo la muda, “ alisema mama Elizabeth Milambo, mkazi wa Kaseke.

Naye Neema Msemakweli alisema anaishukuru Serikali kwa kuwatembelea na kuahidi kuwajengea daraja la muda litakalowwndole kero walizokuwa wakipata hasa mvua inaoinyesha.

“Hapa tulikuwa tukipata taabu sana kuvuka kwenda mashambani mvua zikinyesha na bado tulikuwa tukilipa shilingi 500 hadi 1000 tumefarijika mmekuja na tunamwomba mama Samia Rais wetu ambaye tunajua anatujali wanawake daraja la kudumu kumaliza kabisa tatizo la hapa, “ alisema Neema.

Naye ndugu Innocent Janson, mkazi wa kijiji cha Mbugani, alisema anaomba viongozi waendelee kuwajali wananchi wanyonge kwa kutatua kero zao kwa kuwatembelea katika maeneo yao ili kuona hali halisi ya matatizo yao na alishukuru sana kwa ujio wa mtendaji mkuu wa TARURA na kutoa Suluhu ya kero zao.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa