Friday , 3rd Jun , 2022

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara yake ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuanza kuwavuna Viboko, wanaoonekana kutoka ndani ya Ziwa Victoria na kwenda kurandaranda kwenye makazi ya watu na kufanya mauaji.

Kiboko

Chongolo ametoa maelekezo hayo hii leo Juni 3, 2022, alipowasili kwenye Kijiji cha Nassa wilaya ya Busega mkoani Simiyu kwa ziara yake ya kichama.

"Lakini ninyi wananchi msianze kuwavuna  viboko bila kibali, siku mkiwavuna mniambie na mimi babu yenu nije kuonja nyama yake, nasikia wana nyama tamu sana, siyo," amesema Chongolo