
Mwenyekiti wake wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Ally Mchungahela.
Mchungahela amesema Uchaguzi Mkuu utahusisha nafasi za Rais wa timu, Makamu wa Rais na Wajumbe Watano (5).
Na mchakato wa uchaguzi huo unaanza mara moja ambapo June 5 hadi 9, 2022 zoezi la kuchukua fomu linafunguliwa rasmi likifuatiwa na zoezi la mchujo wa wagombea litakalofanywa kuanzia June 10 hadi 11, 2022 likitekelezwa na Kamati ya Uchaguzi ya Klabu hiyo.
Michakato mingine itaendelea huku ratiba kamili ya michakato hiyo hadi kufikia tarehe rasmi ya zoezi la Uchaguzi Mkuu inatarajiwa kubandikwa katika mbao za matangazo Makao Makuu ya Klabu hiyo.
Kisha nyaraka za Muhtasari na maazimio ya chaguzi hizo ikiwemo Viongozi waliochaguliwa ziwasilishwe Ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Senzo Mbatha Mazingiza.
Mwenyekiti huyo ameyakumbusha matawi yote kuwa viongozi wanaotakiwa kuchaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe Watano lakini pia wachaguliwe Wajumbe wengine Wawili ambao watawakilisha Matawi katika Uchaguzi Mkuu wa July 10, 2022.
Gharama ya kuchukua fomu kwa anayegombea nafasi ya Rais wa klabu na Makamu wa Rais ni Tsh 200,000 kila mmoja, huku wajumbe ikiwa ni Tsh 100,000.
Zoezi hilo likikamilika Young Africans SC itakuwa na Rais wa kwanza kwenye historia, na inakuwa imehama rasmi kwenye mfumo wa zamani.