Saturday , 11th Jun , 2022

Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga umefanya Kikao Cha Wajumbe wake wa Kamati kwa Lengo la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake katika kuwahudumia Wananchi

Akizungumza wakati wa kutoa Pongezi hizo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Hilo Mheshimiwa Sophia Mjema Amesema Wanatambua  mchango  ambao unatolewa na Rais Ambae ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha umoja wa Wanawake Tanzania unakuwa imara, Mshikamano na Upendo wakati wote. 

Mhe. Mjema ameongeza kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa ambae Anamuwakilisha  Mhe.Mama Samia katika kuhakikisha anamsaidia vyema kuusimamia Mkoa Pamoja na Kusimamia Fedha anazozitoa kwaajili  Maendeleo ya Mkoa Kimaendele huo Pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua,

 Katibu wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga Bi. Asha Juma amesema agenda Kuu ni Kumpongeza Rais Samia kwa utendaji wake na jinsi anavyowahudumia Wananchi kwa ustadi na weledi mkubwa hasa kwa mambo Makubwa ambayo ameyafanya kwa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kiasi Cha Fedha alichotoa kwa ajili ya shughuli za Maendeleo kwa kila Halmashauri ndani ya mwaka mmoja Toka ameingia madarakani

Bi. Asha Juma ameongeza kuwa Mama Samia ameweza kumtua Mwanamke ndoo kichwani kwakuomgeza Upatikanaji kwa uRahisi wa Maji katika Mkoa wa Shinyanga. 

Aidha ameongeza kuwa Mhe. Samia ameweza kufanikisha Ujenzi wa Shule za Msingi, Sekondari,Vyuo na Vyuo vya ufundi stadi(Veta) Ambapo  Itasaidia  kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu iliyo Bora .

Rais Ameweza kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za wanawake katika nafasi nyeti na za juu huku akitolea mfano kwa uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dokta Sophia Mjema

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi. Magreti Cosmas amesema Baraza na Jumuiya ya Wanawake wa Ccm Taifa na Mikoa yote wanaungana na Mwenyekiti wao Kitaifa katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa katika kuiletea Tanzania Maendeleo kuanzia kwa Wananchi wake na Kulitangaza Taifa kiujumla.