
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 12, 2022, na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, ambapo amesema tukio hilo imetokea Juni 11, 2022, mtaa wa Kalenga Ilala, kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa 5:40 usiku.
"Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqino (32) raia wa China na baadaye alimfyatulia risasi Fu Nannan alipoteza maisha na Nie anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi,"amesema Kamanda Muliro