Monday , 13th Jun , 2022

Klabu ya Liverpool ya England imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Darwin Nunez wa klabu ya Benfica ya Ureno kwa ada ya uhamisho ya pauni million 85 za England sawa na Bilioni 242 na zaidi ya ,milioni 350 za kitanzania.

(Darwin Nunez akishangilia baada ya kufunga goli)

Liverpool watalipa pesa hiyo kwa awamu mbili kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Ureno. Awamu ya kwanza watalipa pauni million 64 sawa na Bilioni 182 na zaidi ya milioni 285 kwa pesa ya Tanzania na awamu ya pili pauni milioni 21 sawa na Bilioni 59 na zadi ya milioni 781 za kitanzania ambayo Benfica watalipwa kulingana na mafanikio atakayopata Nunez akiwa na Liverpool.

Baada ya kufikia makubaliano hayo ya ada ya uhamisho ya mchezaji huyo kilichobaki ni mchezaji kufanyiwa vipimo vya Afya na kufanya makubaliano binafsi na Liverpool juu ya mshahara na muda wa mkataba atakaosaini ambao unaelezwa utakuwa mkataba wa miaka 6 hadi mwaka 2028.

Nunez raia wa Uruguay ana umri wa miaka 22, msimu uliopita ulikuwa bora sana kwake alifunga mabao 34 na assits 4 kwenye michezo 41 katika mashindano yote, mabao 6 kati ya hayo amefunga kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya na 2 akiwafunga Liverpool. Na kwa ujumla mshambuliaji huyo amefunga mabao 48 kwenye michezo 85 katika misimu miwili akiwa na Benfica.

Usajili huu wa Nunez kujiunga na Liverpool ukikamilika kuna uwezekano mkubwa Sadio Mane akaondoka Liverpool, na tayari Liverpool wamekataa ofa mbili za Bayern Munich za kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 30.