Monday , 13th Jun , 2022

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema zoezi la uwekaji alama kwenywe pori tengefu lililopo tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha linakwenda vizuri hadi sasa

Amewataka wanasiasa kuacha kuwaamasisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kuleta uvunjifu wa amani.

IGP Sirro amesema kufanyika kwa zoezi hilo ni kwa ajili ya manufaa ya Watanzania na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa ujio wa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwenye eneo hilo umesaidia kujenga hamasa na molali kwa askari walioko operesheni hiyo.

Mongella amesema kuwa yote aliyoyashauri yatafanyiwa kazi