Wednesday , 15th Jun , 2022

Basi la kampuni ya Zuberi linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Kahama limepata ajali katika eneo la Mwigumbi Darajani.

Jeshi la Polisi Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya kufanya tathmini kamili

"Ni kweli ajali imetokea na vyombo vya usalama ndio vipo eneo la tukio tutatoa taarifa rasmi baadae" amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, George Kyando