
Tukio hilo limetokea June 10 mwaka 2022 Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya kutuhumiwa kukutwa na viungo vya binadamu maarufu vocha
Waliofikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la mauaji kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ni, Ngalawa Msafiri, Bilali Mohamed, Salimu Halouna, Rajabu Mbarouk, Paulo Jackson, Zulfa Issa, Emmanuel Pallangya na Salimu Rashid
Wengine ni Jonas Harod, Malaki Julius, Salmini Adamu, Ramadhani Husein, Chales Ngole, Athumani Hamad, Ramadhani Amir na Isaya Emmanuel
Akisoma mashitaka hayo mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi Kiteto, Joseph James Soke mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Boniphas Lihamwike alimweleza hakimu huyo kuwa washtakiwa hao walitenda Kosa kinyume na kifungu cha 196 kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walimsababishia kifo Anjel Allon 34, kuwa june 10 mwaka 2022, katika Kijiji cha Engusero Kata ya Engusero kuwa walimpiga hadi kufa mwanamke huyo wakimtuhumu kuwa na viungo vya binadamu
Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo
Kesi hiyo imekuja kwa kutajwa mahamamani hapo na baada ya siku 14 itakuja tena kwa kutajwa