
Kikosi cha timu ya Taifa.
Poulsen amebainisha kuwa anajisikia vibaya na anshindwa kuelewa dhana ya kuinyima timu ya taifa faida ya kufanya mazoezi na maandalizi ya mechi kwenye nyasi halisi za Uwanja wa Mkapa na badala yake wanapelekwa kwenye nyasi za bandia ilihali mchezo dhidi ya Somalia utachezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
“Nashangaa na kiukweli nashindwa kuelewa, kwamba tunapokuwa Taifa Stars tunacheza mchezo wa kufuzu Fainali za CHAN,mchezo muhimu na haturuhusiwi kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa'' amesema Kim Paulsen kocha Mkuu Taifa Stars
Aidha Poulsen amesema kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri isipokuwa beki wa kushoto David Luhende ambaye anasumbuliwa na maumivu ya misuli ambaye amethibitisha kuwa hatahusika kabisa kwenye mchezo huo wa kesho.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya mtoano dhidi ya Somalia ambapo atakayeibuka mshindi atacheza dhidi ya Uganda ili kupata mshindi atakayefuzu kushiriki fainali za CHAN.