
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo wakati alipotembelea mpaka huo leo tarehe 26.07.2022 kuona hali ya usalama katika maeneo hayo kutokan na kuwepo kwa foleni kubwa ya Malori yanayosubiri kufanyiwa ukaguzi.
Kamanda Masejo amesema kuwa hali ya usalama katika mpaka huo ni shwari na hakuna mgomo wowote wa madereva na hawatasita kuwachukulia hatua watu wachache ambao watajaribu kuvunja amani katika eneo hilo kwani vyombo vya dola vipo makini wakati wote.
Kwa upande wake Audax Asheri Afisa Mfawidhi wa Mpaka wa Namanga amesema wanashirikiana na wenzao wa upande wa Kenya kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ili magari yapite vizuri na kuondoa foleni ambayo ipo katika mpaka huo.
Msemaji wa chama cha Wasafirishaji wa Malori Tanzania amesema foleni hiyo inasababishwa na skana ambayo inatumika kukagua magari upande Kenya kuelemewa na wingi wa malori, hivyo akaomba Serikali kwa upande wa Tanzania na Kenya kujadiliana kuona jinsi ya kuboresha upande wa ukaguzi wa malori.