Friday , 29th Jul , 2022

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere, kufuatilia tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 470 zilizojitokeza katika ujenzi wa shule ya sekondari Matui mkoani humo, baada ya yeye kutoridhishwa na ujenzi huo pamoja na kubaini mapungufu.

Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa

Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo mara baada ya diwani wa Kata ya Matui, kumuomba afuatilie kwa undani kuhusu fedha hizo za serikali zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Mbali na hayo, Waziri Bashungwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Manyara ifikapo Januari 2023, kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu Kata hiyo wawe wamesajiliwa na kuendelea na masomo.